Pages

Subscribe:

karibu pata kazi bongo blog, tafadhali tuwezeshe kukidhi haja yako kwa kututumia maoni yako kupitia careendisminder@gmail.com

Mhifadhi wanyamapori, Muhifadhi Mambo Ya Kale, Maafisa Wafugaji Nyuki na Madreva

Wizara Ya Maliasili

Job Description


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/B/40 30 Machi, 2012
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi kwa waajiri mbalimbali katika Utumishi wa Umma kama ifuatavyo:
1.0 MHIFADHI WANYAMAPORI II – NAFASI 130

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Wizara ya Maliasili na Utalii
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi au mbuga za wanyama
 Kusimamia utekelezaji wa utaratibu wa uwindaji na utalii
 Kulinda binadamu na mali zake dhidi ya wanyama hatari.
 Kukusanya na kulinda nyara za Serikali
 Kufanya usafi na ulinzi
 Kubeba na kutunza vifaa vya doria
 Kudhibiti uingiaji na utokaji wa watu na mali kwenye hifadhi
 Kutunza vielelezo vya ushahidi vya nyara
 Kudhibiti wanyamapori waharibifu
 Kukagua vibali na leseni za matumizi ya wanyamapori.
2


Kudhibiti mioto mikali kwenye mapori.

1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kidato cha IV au Kidato cha VI
 Wenye Stashahada/Astashahada ya Uhifadhi wa Wanyamapori kutoka Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
 Waliopitia mafunzo ya nidhamu na ukakamavu yanayotolewa na vyuo vya wanyamapori watapewa kipaumbele. Wale watakaopata nafasi lakini hawana mafunzo hayo, watapewa mafunzo husika kama sehemu ya mafunzo ya “Induction”.
1.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS.B naC kwa mwezi.
2.0 MHIFADHI MAMBO YA KALE II – TGS D – NAFASI 3

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Wizara ya Maliasili na Utalii
2.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kushiriki katika kutunza na kuhifadhi mazingira ya vituo na maeneo ya Mambo ya Kale.
 Kushiriki katika kufanya kazi za ukarabati wa majengo
 Kushiriki katika kuboresha maeneo yenye umuhimu ya kihistoria.
 Kushiriki katika kufanya kazi za ufundi
 Kuratibu na kupokea wageni mbalimbali wanaotembelea Vituo vya Mambo ya Kale.
 Kushiriki katika kufanya utafiti na uhifadhi.
 Kushiriki kuandaa tathmini ya maeneo ambayo yamefanyiwa utafiti na uhifadhi.
 Kuratibu ushauri wa kurekebisha vipengele vya Sheria ya Mambo ya Kale.
 Kuendesha mafunzo ya Elimu ya Jamii kuhusu masuala ya utafiti na uhifadhi kwa njia ya semina, warsha na vipindi vya radio.
 Kushiriki katika kuandaa vipindi vya TV na Radio
 Kushiriki katika kuandaa kazi za maabara.
 Kushiriki katika kuandaa kumbukumbu za mambo ya kale.

2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Shahada/stashahada ya juu ya Sayansi ya Jamii au Sayansi ya Asili, waliojiimarisha (major) katika mojawapo ya michepuo ya Jiologia, elimu ya viumbe, Akiolojia, Anthropolojia, Jiografia, Historia, Paleontolojia au Ethnolojia kutoka Vyuo vinavyotambulika na Serikali.

2.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi. 3


3.0 AFISA UFUGAJI NYUKI II (WAKUFUNZI) – TGS D – NAFASI 10

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Wizara ya Maliasili na Utalii
3.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kusimamia uanzishaji wa hifadhi za nyuki na manzuki.
 Kutangaza sera na Sheria za ufugaji nyuki.
 Kufundisha masomo ya fani ya ufugaji nyuki.
 Kukusanya takwimu za raslimali na ufugaji nyuki
 Kupanga na kupima ubora wa mazao ya nyuki.
 Kutayarisha mpango wa kazi (Scheme of Work) wa mafunzo.
 Kufundisha masomo ya fani husika.
 Kupima maendeleo ya Wakurufunzi katika nadharia na vitendo.
 Kutunga na kusahihisha mitihani.
 Kusimamia mitihani katika vyuo vya Maliasili.

3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Shahada katika fani ya Ufugaji Nyuki au Sayansi ya Elimu ya Mimea, Elimu ya wadudu au Elimu ya Wanyama kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na serikali.

3.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.
4.0 DEREVA DARAJA LA II (DRIVER II) – NAFASI 7

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Wizara ya Maliasili na Utalii
4.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuendesha magari ya abiria, magari madogo na malori
 Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote, na kufanya uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo,
 Kufanya matengenezo madogo madogo katika gari,
 Kutunza na kuandika daftari la safari “Log-book” kwa safari zote.

4.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV, Wenye Leseni daraja la “C” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali na wenye Cheti cha Majaribio ya ufundi Daraja la II.
4.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi. 4

NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. WAAJIRI WOTE WALIOPO NJE YA DAR ES SALAAM WANAOMBWA KUSAMBAZA MATANGAZO HAYA KWENYE MBAO ZA MATANGAZO NA MAENEO MENGINE.
xiii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 13 Aprili, 2012
xiv. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.

Katibu,
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma,
SLP.63100,
Dar es Salaam. 5

AU
Secretary,
Public Service Recruitment Secretariat,
P.O.Box 63100
Dar es Salaam.

0 comments:

Post a Comment